Mahitaji
- Viazi ulaya 4 vya wastani
- Hoho jekundu 1/2
- Hoho la njano 1/2
- Hoho la kiajani 1/2
- Njegere 1 kikombe cha chai
- Carrot 1 kubwa
- Broccoli kidogo
- Cauliflower kidogo
- Kitunguu 1
- Nyanya 1/2 kopo
- Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula
- Curry power 1 kijiko cha chakula
- Coriander powder 1 kijiko cha chai
- Tarmaric 1/2 kijiko cha chai
- Olive oil
- Chumvi
- 1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
0 Comments
Post a Comment