Mahitaji

  • Machungwa 3
  • Karoti 2
  • Peach 1
  • Asali (ONYO: USITUMIE ASALI KWA MTOTO CHINI YA MWAKA MMOJA)

Maelekezo

  • Kamua chungwa vizuri kisha hifadhi kwenye chombo safi pembeni.
  • Menya karoti kisha kata vipande vidogo vidogo. Weka kwenye jagi la kusagia  (blender).
  • Menya peach, kata vipande vidogo vidogo kisha toa mbegu. Changanya na karoti kwenye jagi.
  • Changanya juisi ya chungwa kwenye jagi, hii inasaidia kutumika kama kilainishi.
  • Saga vizuri hadi vipondeke na kuwa laini kabisa.
  • Tumia chujio, chuja juisi vizuri kwenye chombo safi, mfano bakuli.
  • Mie nimeongeza asali, lakini siyo lazima kuongeza asali, maana juisi kama ilivyo ni tamu. Kabla hujaongeza asali zingatia umri wa watoto wanaokunywa hii juisi.

ZINGATIA: Usimpe asali mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja. Asali huweza kubeba vijidudu hatarishi kwa mtoto mchanga ambavyo husababisha ugonjwa unaoitwa Botulism.

UMUHIMU

Juisi hii ina mchanganyiko wa matunda, hivyo ina virutubisho vingi zaidi vya asili. Kati ya faida chache ni kama hizi:

  • Chanzo cha vitamin C (Chungwa)
  • Kuboresha kinga ya mwili (Peach)
  • Kuifanya ngozi kunawiri (Peach, karoti)
  • Kuimarisha moyo na macho (Peach, karoti)
  • Kusafisha damu (Chungwa, karoti)
  • Kuboresha mmeng’enyo wa chakula (Karoti)