Mahitaji
- Mchele ½ kilo
- Binzano ya njano kijiko 1 kikubwa
- Vitunguu maji 2
- Binzari nyembamba kijiko 1 chai
- Iliki kijiko 1 kikubwa, twanga ½ na nyingine weka ikiwa nzima
- Gram masala ½ kijiko cha chai
- Mafuta vijiko 3 vikubwa
- Hing kijiko 1 kidogo
- Chumvi kijiko 1 kidogo
- Mdalasini kijiko 1 kidogo
- Tangawizi ya unga kijiko 1 kidogo
Maelekezo
Chakula rahisi kuandaa na chenye utamu wa kipekee. Unaweza kuongeza viungo unavyopenda ili kuongeza ladha ya chakula.
- Andaa viungo – menya na vitunguu.
- Weka mafuta yakipata moto, weka kitunguu maji. Angalia kisiive sana, kisha weka viungo vyote na koroga vizuri. Baada ya dakika 2, weka mchele na chumvi kisha koroga.
- Weka maji ya moto kiasi funika, hakikisha mvuke hautoki. Punguza moto uwe mdogo sana.
- Baada ya dakika 15, funua chakula, geuza na onja kama wali wa chini umeanza kuiva au umeiva kabisa. Ukiwa umeiva weka vijiko 3 vya maji, funika. Baada ya muda geuza.
- Baada ya dakika 5 unaweza kuepua na kujiramba.
Unaweza kula chakula hiki mchana au usiku. Ni chakula muafaka kwa familia, lakini punguza viungo vikali kama kuna watoto wadogo wanaokula pia hiki chakula.
0 Comments
Post a Comment