Mahitaji

Kwa nyama

  • Chumvi
  • Tangawizi
  • Nyama ½ kilo (Vizuri kama itakuwa steki)
  • Pilipili hoho 2 (Kijani na nyekundu)
  • Miti ya mishikaki

Kwa sauce ya kulowekea nyama (marinade)

  • Kitunguu saumu 1, kimenywe na kupondwa vizuri. Au tumia cha unga.
  • Limao 1
  • Tandoori (Hii inapatikana sana kwenye maduka yauzayo viungo vya chakula vya kihindi)
  • Maggi cube
  • Sweet pepper au capsicum (Ni pilipili kama hoho maana haina ukali, na ni unga unga, utapata kwenye maduka yanayouza viungo vya chakula zaidi kwa wahindi)
  • Mafuta ya kula vijiko 2 vikubwa (Nimetumia olive oil)

Maelekezo

Ukimaliza kuandaa mishikaki yako itakuwa hivi:

misosi-mishikaki-oven

Andaa sauce ya kuloweka nyama (Marinade):

  • Changanya kila kitu pamoja – kitunguu saumu, sweet pepper, tandoori, maggi cube na mafuta ya kula. Kata limao kisha kamulia. Kwenye mchanganyiko. Koroga pamoja hadi ichanganyike vizuri kabisa.  Hifadhi pembeni.

misosi-mishikaki-marinade

Andaa nyama:

  • Kata nyama kwenye vipande vya wastani, visiwe vidogo sana maana vitaungua. Osha na kisha hifadhi pembeni.
  • Kata pilipili hoho, karoti vipade vyenye ukubwa wa wastani.

misosi-mishikaki5

  • Anza kutunga mishikaki kwa kuweka nyama na mboga mboga pamoja.

misosi-mishikaki6

  • Mwagia sauce juu ya mishikaki iliyo tayari. Paka vizuri hadi sauce iingie kila sehemu. Hifadhi kwenye chombo safi na weka kwenye jokofu (fridge) kwa muda wa masaa mawili ili vipate kuchanganyika.

misosi-mishikaki7

  • Muda ukifika, washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (185°C) kwa dakika 10. Kisha weka mishikaki kwenye waya wa oven. Geuza mara kwa mara ili mishikaki isiungue. Baada ya dakika 30 hadi 40 itakuwa tayari.
  • Jirambe na mishikaki mitamu.

misosi-mishikaki2

misosi-mishikaki-oven