Mahitaji
·
Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe
vya chai)
·
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha
chai)
·
Hamira (dried yeast 3/4 kijiko
cha chakula)
·
Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko
cha chai)
·
Ute wa yai 1(egg white)
·
Tui la nazi (coconut milk kikombe 1
na 1/2 cha chai)
·
Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Changanya unga wa mchele, hamira,
hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri.
Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua
kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri.
Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200°C kisha chukua chombo cha
kuokea na ukipake mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie katika oven
na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na
chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.
0 Comments
Post a Comment