Mahitaji
- Nyanya
- Pilipili hoho
- Vitunguu maji
- Vitunguuswaumu
- Carrots
- Ndimu
- Nazi (tui zito)
- Chumvi
- Samaki
- Tangawizi
Maelekezo
- Andaa viungo – tangawizi, ndimu, vitunguu saumu – menya, kata na ponda kama inawezekana.
- Osha samaki vizuri kisha mloweke kwenye viungo (chaganya tangawizi,ndimu,vitunguu saumu na chumvi) kwa muda wa saa moja.
- Andaa viungo vyako mbadala – nyanya,vitunguu,karoti, na pilipili hoho. Tengeneza tui zito la nazi na hifadhi pembeni.
- Bandika kikaangio, au sufuria jikoni, weka mafuta ya kula na acha yapate moto.
- Weka samaki. Kaanga samaki ila hakikisha asikauke sana.
- Fanya hivyo kwa samaki wote waliobaki.
- Bandika sufuria jikoni weka mafuta kiasi – unaweza pia kutumia uliyokaangia samaki
- Mafuta yakipata moto, weka vitunguu maji kisha koroga hadi kibadilike rangi kiwe rangi ya udongo.
- Weka kitunguu saumu kisha koroga kidogo kama dakika 1
- Weka pilipili hoho na karoti. Koroga kiasi, kwa takribani dakika 2.
- Weka nyanya, koroga kiasi ili zichanganyike vizuri. Funika na mfuniko na acha ziive kwa mvuke.
- Nyanya zikiiva, weka tui zito liache lichemke kama dakika 10.Mchuzi ukiwa mzito weka samaki na koroga mpaka samaki achanganyikane na viungo vizuri. Acha jikoni kwa dakika takribani 3 nakisha ipua.
- Hapo msosi utakua tayari
0 Comments
Post a Comment